Unataka kutoa taarifa kuhusu nini?

Hii ni nini

Unaweza kuripoti kwetu sisi picha za unyanyasaji wa kingono kwa mtoto, zinazopatikana katika tovuti yoyote ulimwenguni.

Hii inajumuisha picha zinazomuonesha mtoto katika mkao wa kingono; mtoto akijichua mwenyewe; akiingiliwa kimwili, akitomaswa au kufanyiwa matendo yoyote yanayopelekea ngono kati ya watoto kwa watoto ama mtoto na mtu mzima ama yanayohusisha watoto na wanyama.

Taarifa zaidi

Uliona wapi taarifa hizi?

Maelezo ya tovuti

Ili tuweze kuichunguza tovuti tunahitaji anwani kamili ambayo inafahamika kama URL mf. http://www.iwf.org.uk/what-we-do, www.iwf.org.uk/what-we-do au iwf.org.uk/what-we-do. Hii inapatikana juu ya ukurasa.

Iwapo una taarifa yoyote unayodhani itatusaidia kama maelezo ya wapi maudhui unayoyatolea taarifa yanapatikana, kwenye tovuti kubwa au jina linalotumika na neno la siri linaloitajika kuweza kuigia, tafadhali ambatanisha kwenye sanduku la maelezo.

Kama ungependai kutoa taarifa kuhusu tovuti nyingine tafadhali jaza ripoti/fomu mpya. Tafadhali usiweke kiungo kwenye sanduku; kufanya hivyo hazitashughulikiwa.

Asante.

Maelezo ya barua pepe

Barua pepe zisizo halali ‘SPAM’ zilizoorodheshwa hapo chini zilishatolewa taarifa, hivyo huna haja ya kuzitolea taarifa tena, tafadhali zifute tu kwenye barua pepe yako kumaliza taarifa hii.

  • Porno with 3 **
  • Here you can download the ** and... ** **
  • Here you can download the **** lorem
  • ** **, and real **** on the streets
  • Download the ** and** **!!! and real ****
  • Porno with **, Here you can download the ** and...
  • Here you can download the **** lorem ** **, and real

Kama barua pepe unayoitolea taarifa haijaorodheshwa hapo juu tafadhali endelea na hatua inayofuata.

Maelezo ya barua pepe

Kutoa taarifa ya barua pepe isiyohalali ‘SPAM’ tunahitaji kiunganishi ‘LINK’ iliyoambatanishwa kwenye barua pepe.

Anwani ya tovuti iko kama hii: http://www.iwf.org.uk au www.iwf.org.uk

Tafadhali tafuta ushauri kama unahitaji utaratibu wa kutafuta anwani ya tovuti au tumia msaada wa makala ya barua pepe uliyotumiwa.

Kama huna uhakika wa jinsi ya kufanya zoezi hili tafadhali tutumie ‘FORWARD’ barua pepe unoyoitolea taarifa kwenye anuani yetu [email protected]

Taarifa ya jarida la habari

Newsgroups' ni majukwaa ya dondoo za habari yanayotumiwa kuzungumza mada maalum. Watumiaji wa 'Newsgroup' huwasiliana kupitia huduma ijulikanayo kama 'UseNet' ambayo ilikuwepo kabla ya mitandao tunayoitumia kwa sasa. Hata hivyo, baadhi ya 'Newsgroups' bado zinatumiwa na zina uwezo hata wa kubeba faili za picha / video.

Ukiwa unatoa taarifa ya picha/jarida lililopo kwenye kikundi cha habari tafadhali weka taarifa za kutosha kadri uwezavyo, kwa mfano:

  • Jina la kundi - alt.binaries.example.example
  • Jina la kundi - [email protected]:
  • Kichwa cha habari ya unachotuma - Mkusanyo wa picha:
  • makala - [email protected]:
  • Tarehe - 01/01/2013:
  • Vyanzo vya habari - examplefeed:

Tafadhali ongeza taarifa nyingine yoyote unayodhani inafaa kwenye sanduku la maelezo.

Iwapo taarifa yako haihusiani na kitu ambacho kipo hadharani mtandaoni sisi tutashindwa kuchukua hatua, yaweza kuwa suala la polisi.

Kama taarifa yako inahusiana na mambo yafuatayo hapo chini, tafadhali wasiliana na Dawati la Jinsia na Watoto Polisi lililopo karibu na wewe au piga namba 116 simu ya bure ya Huduma kwa Mtoto.

  1. Unahisi mtoto anafanyiwa ukatili.
  2. Picha zilizohifadhiwa kwenye vifaa binafsi vya kielektroniki kama simu ya mkononi, kompyuta au tableti.
  3. Maandishi yasiyo na picha kupitia mitandao ya kijamii (mitandao ya kuchat/kuwasiliana).
  4. Usambazaji wa majalada kupitia mitandao ya makundi/marafiki au kwa huduma za upakuaji mtandaoni.

Unataka kuficha utambulisho wako?

Taarifa zako zitahifadhiwa faraghani

Kama ungependa utambulisho wako ubaki siri, hilo linawezekana.

Lakini kama ungependa kujua hatma ya taarifa uliyotoa basi tutahitaji barua pepe yako ili tuweze kukutumia uthibitisho wa taarifa yenye namba maalumu ya kumbukumbu.

Namna hii, utaweza kuwasiliana nasi kwa taarifa zaidi juu ya taarifa uliyotoa, nasi tutawasiliana nawe endapo tutahitaji taarifa zaidi.

Taarifa zako

  • Endapo utatoa taarifa zako zitahifadhiwa kwenye kumbukumbu za tovuti ya IWF kwa miezi mitatu ili kukufikia kwa taarifa zaidi.
  • Baada ya hapo zitafutwa kulingana na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa.
  • Tunakuhakikishia taarifa zako hazitawekwa wazi kwa watu wengine bila ruhusa yako ya maandishi. Hata hivyo wakati ambapo taarifa zako zinaweza kuwa muhimu kwetu ili kuzifikisha katika kituo cha polisi au kwa vyombo vya kimataifa vya kisheria ili ziweze kuwasaidia katika kufanya uchunguzi na endapo kutokufanya hivyo kutasababisha uwezekano wa mtoto au watu wengine kupata madhara makubwa. Kwa mantiki hiyo utoaji wa taarifa utazingatia maslahi ya umma au maslahi mapana yenye madhumuni ya kuzuia usambaaji wa taarifa za unyanyasaji wa kingono kwa mtoto.

Si votre signalement ne concerne aucune des options listées ci-dessus, veuillez contacter les forces de police.